Jinsi ya kuongeza gharama
Ongeza gharama mtu anapolipia kitu ambacho kikundi kinagawana. SplitEase husasisha salio la kila mtu mara tu unapohifadhi.
Hatua
- Gusa kitufe cha + katikati ya upau wa vichupo, au fungua kikundi na uguse Ongeza gharama (Add expense).
- Hakikisha kikundi kilicho juu ni sahihi, kisha weka Kiasi (Amount) na gharama ilikuwa ya nini.
- Chini ya Imelipwa na (Paid by), chagua aliyelipa.
- Chini ya Gawanya (Split), chagua wanaogawana gharama na jinsi gani. Kwa chaguomsingi, gharama hugawanywa sawa kwa sawa.
- Gusa Hifadhi (Save).
SplitEase hupendekeza aina ya gharama kutokana na maelezo. Unaweza kuibadilisha kabla ya kuhifadhi.
Ili kulipa kwa sarafu nyingine, gusa alama ya sarafu karibu na kiasi.
Programu ya SplitEase bado haipatikani kwa lugha hii. Majina ya vitufe yaliyo kwenye mabano ndiyo utakayoyaona kwenye skrini.