SplitEase+

Jinsi ya kuchanganua risiti ili kuongeza gharama

Kuchanganua risiti husoma jumla na maelezo kutoka kwenye bili ili usilazimike kuyaandika. Ni sehemu ya SplitEase+.

Hatua

  1. Gusa kitufe cha +, kisha Changanua (Scan).
  2. Piga picha ya bili nzima, au chagua Picha (Library) au PDF ili kutumia faili ulilonalo tayari.
  3. Kagua maelezo ambayo SplitEase imepata na uguse Tumia (Use).
  4. Kagua aliyelipa na jinsi ilivyogawanywa, kisha gusa Hifadhi (Save).

Picha hupakiwa kwenye SplitEase ili isomwe. Soma Sera ya Faragha yetu kujua jinsi inavyoshughulikiwa.

Uchanganuzi unaweza kukosea. Hakiki kiasi kila mara kabla ya kuhifadhi.

Programu ya SplitEase bado haipatikani kwa lugha hii. Majina ya vitufe yaliyo kwenye mabano ndiyo utakayoyaona kwenye skrini.

Maswali yanayohusiana

Bado unahitaji msaada?

Tuandikie na mtu kutoka timu ya SplitEase atakujibu.

Wasiliana na huduma kwa wateja
Lugha: Kiswahili