SplitEase+

Jinsi ya kuweka gharama inayojirudia

Gharama inayojirudia huongezwa kwenye kikundi kiotomatiki tarehe yake ikifika, ikigawanywa kama ulivyoiweka. Ni sehemu ya SplitEase+.

Hatua

  1. Fungua kikundi, kisha Mipangilio ya kikundi (Group settings).
  2. Gusa Gharama zinazojirudia (Recurring expenses), kisha Ongeza (Add).
  3. Weka kiasi, anayelipa na jinsi inavyogawanywa, kisha chagua inajirudia mara ngapi: kila siku, kila wiki, kila mwezi au kila mwaka.
  4. Gusa Hifadhi (Save).

Ili kuruka mara moja, fungua gharama inayojirudia na uguse Ruka inayofuata (Skip the next occurrence). Ratiba inaendelea baada ya hapo.

Programu ya SplitEase bado haipatikani kwa lugha hii. Majina ya vitufe yaliyo kwenye mabano ndiyo utakayoyaona kwenye skrini.

Maswali yanayohusiana

Bado unahitaji msaada?

Tuandikie na mtu kutoka timu ya SplitEase atakujibu.

Wasiliana na huduma kwa wateja
Lugha: Kiswahili