Jinsi ya kumalizana na mtu

SplitEase hufuatilia nani anadaiwa na nani, lakini haishughulikii malipo. Mlipe mtu huyo kwa njia unayotumia kawaida, kisha urekodi malipo kwenye programu ili salio la wote wawili lisasishwe.

Hatua

  1. Fungua kikundi na uguse Malizana (Settle up).
  2. Ikiwa umemlipa mtu, gusa Rekodi malipo (Record payment) karibu na jina lake, hakiki kiasi na uthibitishe. Unaweza kurekodi sehemu tu ya deni lako.
  3. Ikiwa mtu amekulipa, gusa Weka alama kuwa imepokelewa (Mark as received) karibu na jina lake na uthibitishe.

Ili kuona malipo ya awali, gusa Historia (History) kwenye skrini hiyo hiyo.

Programu ya SplitEase bado haipatikani kwa lugha hii. Majina ya vitufe yaliyo kwenye mabano ndiyo utakayoyaona kwenye skrini.

Maswali yanayohusiana

Bado unahitaji msaada?

Tuandikie na mtu kutoka timu ya SplitEase atakujibu.

Wasiliana na huduma kwa wateja
Lugha: Kiswahili